Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.

Marko 1:15

TUBUNI

Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.

Warumi 3:23

DHAMBI

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Warumi 6:23

MAUTI

Lakini Mungu aonyesha pendo lake kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa bado wenye dhambi.

Warumi 5:8

UPENDO

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

Waefeso 2:8-9

IMANI

Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Warumi 10:9-10

UZIMA

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya.

2 Wakorintho 5:17

MPYA KATIKA KRISTO