kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

Warumi 3:23

DHAMBI

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Warumi 6:23

KIFO

Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu. Warumi 5:8

UPENDO

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote asije akajisifu juu ya wokovu wake.

Waefeso 2:8-9

IMANI

Kama ukikiri kwa kinywa chako kuwa Yesu ni Bwana na ukiamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Kwa maana mtu ana poamini moyoni mwake huhesabiwa haki, na anapokiri kwa kinywa chake, huokolewa.

Warumi 10:9-10

UZIMA

Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja.

2 Wakorintho 5:17-19

MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO